Meneja wa soka kutoka nchini Ureno, Jose Mourinho ameendelea kuonyesha makeke ambayo yanadhihirisha huenda akawa mkuu wa benchi la ufundi la Man Utd ambayo inatajwa kuwa mbioni kuachana na Louis Van Gaal.

Mourinho, ameendelea kuonyesha ishara huenda akawa meneja wa klabu hiyo yenye mafanikio katika soka la nchini England, kufuatia kauli aliyoitoa ya kuwa tayari kufanya kazi na baadhi ya wachezaji waliopo kikosini huko Old Trafford.

Akizungumzia muelekeo wa maisha yake baada ya msimu huu, Mourinho amesema hatopendezwa na hatua ya kufanya kazi na viungo Juan Mata mwenye thamani ya pauni milioni 37 na Marouane Fellaini aliyenunuliwa kwa pauni milioni 27 akitokea Everton miaka mitatu iliyopita.

Amesema tayari ameshaliwakilisha hilo kwa kiongozi mkuu wa Man Utd  Ed Woodward, wakati wakizungumzia masuala mbali mbali ya maisha ya soka nje na ndani ya uwanja.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza linaandika kuwa, Mourinho ambaye hakuwahi kuficha utashi wake wa kuwa meneja wa Man Utd, ametoa picha ya kikosi anachokihitaji katika kikao chake na Woodward.

Antoine Griezmann Aifungia Vioo Chelsea
Vibosile Wa Liverpool Wafunga Breki Kwa Mashabiki