Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Atletico Madrid ya Hispania, Antoine Griezmann ameikataa Chelsea kwa kutuma salamu ya kutaka kubaki mjini Madrid.

Griezmann ambaye alijiunga na Atletico Madrid mwaka 2014 baada ya fainali za kombe la dunia zilizounguruma nchini Brazil, akitokea Real Sociedad, amewasilisha salamu hizo huko magharibi mwa jijini London, kutokana na taarifa za kuhitajika Stamford Bridge kuendelea kuchukua nafasi katika vyombo vya habari siku hadi siku.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amesema bado ana malengo makubwa ya kuendelea kubaki Atletico Madrid, na anaamini yatatimia chini ya ukufunzi wa meneja Diego Simeone.

“Ninajihisi mwenye furaha, na nipo sehemu tulivu ya kucheza soka langu kwa sasa,”

“Ninataka kuendelea kubaki hapa, nadhani hata klabu haina mpango wa kuniunza, hivyo siondoki” alisema Griezmann

Rais wa Atletico Enrique Cerezo, hivi karibuni alikanusha suala la Griezmann kuwa mbioni kuuzwa huku akidai hakuna mazungumzo yoyote ya uhamisho.

Dimitri Payet Awafunga Midomo Viongozi Wa Man City
Jose Mourinho Awaweka Sokoni Juan Mata, Marouane Fellaini