Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya West Ham Utd ya England, Dimitri Payet amejitia kitanzi cha kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo kwa sasa inanolewa na meneja kutoka nchini Croatia, Slaven Bilic.

Payet ambaye ni msaada mkubwa kwa sasa katika kikosi cha West Ham Utd, amekubalia kusaini mkataba mpya ambao una tahamani ya pauni milioni 35 na utakua mnono katika historia ya klabu hiyo.

Hatua hiyo inafuta mipango ya klabu ya Man city, ambayo ilikua katika rada za kutaka kumnasa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, mwishoni mwa msimu huu.

Payet amejitia kitanzi cha miaka mitano na nusu katika mkataba huo ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa pauni 125,000 kwa juma.

Payet is all smiles as he agrees his new deal with Premier League side West Ham on Thursday nightPayet akitabasamu wakati akisaini mkataba mpya 

Mchanganuo wa dili lake unaonyesha atalipwa mshahara wa wa pauni 68,000 kwa juma, pauni 25,000 kwa juma endapo atakua sehemu ya kikosi pamoja na pauni milioni 1 kama dau la kusaini mkataba mpya sambamba na marupurupu mengine kwa juma.

Utafiti: Umaarufu wa Lowassa waporomoka kiasi hiki
Antoine Griezmann Aifungia Vioo Chelsea