Kamanda wa Polisi moka wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kumkamata Benson Bernard (31) na kuanza hatua za kushirikiana na madaktari ketengo cha afya ya akili kumchunguza baada ya kutaka kuzamisha mtoto wake mtoni wakiwa watupu.

Kamanda Mutafungwa ametoa kauli hiyo leo jumamosi Desemba 21, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari wakati akizungumzia tukio hilo kama alivyokuwa ameahidi kufanya.

Tukio hilo limetokea Desemba 19, 2019 katika Maporomoko ya Maji ya Nguzi Camp mkoani Morogoro, na taarifa zinaeleza kuwa wakati mtu huyo akiwa katika Maporomoko hayo, Askari waliokuwa katika shughuli nyingine walimuona na kumtilia shaka.

Inadaiwa kuwa, baada ya kuonekana alijitosa kwenye maji ya kina kirefu akiwa na mtoto huyo ambaye alikuwa akipiga kelele na kusema “baba unaniua, baba unaniua” ,….Bofya hapa kutazama ilivyokuwa

Wataalam wa mipango waagizwa mawazo ya ubunifu
Kiwanda cha nyama ya Punda chaadhibiwa uchafuzi wa Mazingira