Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga imekitoza faini ya ya Tsh. 500,000/= kiwanda cha nyama ya punda, Fang Hua na kukipa muda wa siku saba kurekebisha kasoro zilizopo kwenye kiwanda hicho.

Kiwanda hicho kipo eneo la Ibadakuli manispaa ya Shinyanga na kinamilikiwa na wawekezaji raia wa China, kimekumbwa na adhabu hiyo baada ya kukutwa na makosa ya uchafuzi wa mazingira kama kutoa harufu kali na kutozingatia baadhi ya taratibu za uhifadhi wa mazingira.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko ametangaza hatua hiyo juzi baada ya kufanya ziara ya ukaguzi kufuatia kupokea malalamiko ya wananchi ambao walidai kuchoshwa na harufu kali ya kiwanda hicho.

DC, Mboneko amesema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kuamua kufanya ziara ili ajionee mwenyewe na amethibitisha kukutana na hali ambayo haikumridhisha.

” Nilipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka kiwanda hicho kwamba kuna harufu kali sana ambayo imekuwa kero, nimeamua niamkie hapa kukagua kujiridhisha kwamba kipo kwenye hali gani” alisisitiza DC, Mboneko.

 

Video: Akutwa mtoni na mtoto akiwa na silaha bila mavazi
Wafariki kwa kuchoma dawa za Mganga mgodini