Taarifa zilizotolewa leo Disemba 20, 2019, na kituo cha haki za binadamu, (LHRC) zimeeleza kuwa afisa wao wa kitengo cha elimu kwa umma, Tito Magoti, amekamatwa kwa nguvu na watu watano ambao hawakuweza kutambulika mara moja maeneo ya Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Anna Henga ameeleza kuwa leo majira ya saa nne asubuhi Magoti alifika Mwenge kwa lengo la kununa simu kabla ya kukamatwa na watu waliokuwa kwenye gari na kuelekea posta.

” Tito Magoti amechukuliwa kwa mabavu na watu wasiojulikana mnamo Disemba 20 mwaka 2019 majira ya saa nne asubuhi eneo la Mwenge Jijini Dar es salaam ambapo alifika kwa lengo la kujinunulia simu” imeeleza taarifa hiyo.

Na kuongeza kuwa ” mashuhuda wamearifu kuwa watu waliomchukua walikuwa katika gari aina ya Harrier rangi ya maziwa baada ya kumchukua walielekea uelekeo wa Posta, Dar es salaam”

Aidha kituo hicho kimetoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama hususani jeshi la polisi kuendelea kuchukua hatua za kudhibiti mwendelezo wa matukio ya watu kutekwa bila watekaji kufahamika.

Video: Uteuzi wa Mnyika watikisa, Kigogo mwingine aunganishwa kesi ya Sethi, Rugemalira
TCRA: Laini zisizosajiliwa kufungwa baada ya Desemba 31