Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka wazi maagizo aliyopewa na Hayati Benjamin Mkapa juu ya sehemu anayohitaji kuzikwa siku umauti utakapo mfika.

Amesema Mkapa alikataa kuzikwa Dodoma katika eneo ambalo wananchi waliwatengea viongozi na akaagiza azikwe kijijini kwao Lupaso.

Hivyo basi ametangaza kuwarudishia wananchi wa Jiji la Dodoma eneo lililokuwa limetengwa maalumu kwa mazishi ya maraisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye ibada ya mwisho ya mazishi ya Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamini Mkapa leo, Julai 29, 2020, na kusisitiza kuwa ni vyema sehemu ya kipande cha eneo hilo akazikwa kiongozi mstaafu John Samuel Malecela ambaye Dodoma ndiyo nyumbani kwao…, Bofya hapa kutazama

Kondomu zilizokosa viwango zaondolewa sokoni
Polisi walivyozuia ndoa ya mwanafunzi katavi