Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Adam Fimbo amebainisha kuwa mwaka wa fedha 2019/2020 mamlaka imeondoa kondomu 17,076 kwa kushindwa kukidhi matakwa ya viwango vya bidhaa.

Amesema TMDA huchunguza kondomu kabla ya kuingia sokoni kwa kupima ubora wake kama kiwango cha mafuta, ustahimili wa matumizi na urefu wake, endapo ikikutwa haina vigezo haiingii sokoni.

Aidha amesema TMDA inafanya kazi ya uthibiti na ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha afya ya wananchi inakuwa salama.

Aina ya kondomu zilizotolewa mtandaoni ni aina tano ya kondomu life guard, ultimate, maximum classic, prudence na chishango.

Ikumbukwe kuwa mwaka wa 2019 shirika la Marie stopes liliagiza kuondolewa zaidi ya kondomu milioni moja kutoka madukani nchini Uganda baada ya kugunduliwa kwamba mipira hiyo ilikuwa haikithi viwango na haifai kutumika kabisa.

Maktaba ya kisasa kujengwa Lupaso
Video: Alichoagiza Mkapa juu ya mazishi yake ''Nisizikwe Dodoma''