Leo Novemba 28, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu Ikulu jijini Dar es salaam , ambapo mazungumzo hayo yamehusisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.

Baada ya mazungumzo hayo waliongea na waandishi wa habari ambapo kati ya mambo aliyozungumzia Rais Magufuli ni kuhusu bomba la TAZAMA kupunguza uwezo wa kusafirisha mafuta, ikiwa ni swali lililoulizwa na mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten cha jijini Dar es salaam.

Video: Sakaya amgeukia Tulia Ackson, asema Bunge linahitaji hekima si sheria tu
Waitara: Makonda toa ushahidi kuhusu tuhuma za Sirro