Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema anawahikishia watanzania na wote walioguswa na tetemeko la ardhi Kagera kuwa fedha zote zilizochangwa zitawafikia wahusika kama Serikali ilivyoahidi kusimamia mwenendo wa uingiaji wa michango na utokaji wa michango hiyo.

Majaliwa amesema hatua iliyochukuliwa na Serikali kwa kuwasimamisha na kutengua uteuzi wa Watumishi 3 na Watumishi 2 wa CRDB ni kudhibitisha kwamba kweli Serikali inasimamia mwenendo wa uingiaji wa michango na utokaji wa michango hiyo.

Amesema Watumishi hau walifanya ujanja kufungua akaunti ya sili ambayo ilikuwa ikipokea fedha na kutoka siku hiyo hiyo, huku kukiwa na zuio la kutoa fedha kabla ya wakati ambao Serikali itaridhia fedha zitolewe.

Majaliwa apokea jumla ya sh. mil.190 kutoka Pakistani na wengine, Tetemeko Kagera
Majaliwa apokea zaidi ya sh. mil. 760 kwa ajili ya waathirika tetemeko Kagera