Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema leo Oktoba 18, 2016 amekabidhi soko la samaki, Feri katika uongozi mpya ambao utakuwa ukisimamia soko hilo. Wakati akisoma taarifa iliyoandaliwa na uongozi wa awali aligundua utaratibu mbovu wa ulipaji ushuru kwa wafanyabiashara katika soko hilo.

Mjema ameonyesha kuwa na wasiwasi na taarifa hiyo iliyoonyesha utaratibu wa ushuru kutoendana na watu husika katika soko hilo.

Kufuatia hayo, Mkuu wa Wilaya ameutaka uongozi mpya kuaangalia upya utaratibu wa utozaji ushuru kwa wafanyabiashara, pia kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya soko hilo ikiwa ni pamoja na kulifanya kuwa la kimataifa tofauti na lilivyo kwa sasa kwani halina ahadhi ya kuitwa soko la kimataifa. Bofya hapa kutazama video

Video: Godbless Lema avuruga hotuba ya RC Gambo
Miamba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara Kupepetana Juma Hili