Rapa Dee Pesa ambaye amekuwa akifanya mtindo unaoweza kuubatiza jina la ‘African Trap’ amefunguka kuhusu wimbo wake mpya wa ‘Bless’ ambao umeyachukua matukio mengi yanayoonesha imani za kishirikina.

Dee Pesa ambaye alikutana na kamera za Dar24 na kufanya mahojiano maalum, alieleza jinsi ambavyo alishindanisha nguvu za giza na nguvu za kiroho za mcha Mungu kwenye wimbo huo uliopikwa na Elly Dabway.

Rapa huyo ambaye aliwahi kufyatua wimbo wa ‘Kanjibahi’ amewataja mweusi G-Nako na Cpwaa kwenye awamu nyingine ya wimbo huo.

Dee Pesa na Elly Dabway kwenye mahojiano hayo wamefunguka mengi walipoketi ndani ya studio za Dar24, angalia hapa uyapate yote.

Video: Chin Bees Afyatua Kombora la Kuwaamsha Waliokaa, ‘Nyonga Nyonga’
The Ins and Outs of College Midterm Papers