Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameahidi kuhamishia Dodoma Serikali yote, Rais ameongea hayo katika mkutano wa kukabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM baada ya kupigiwa kura za ndio 2398 sawa na asilimia mia moja kutoka kwa wanachama wa chama hicho.

Mambo ambayo Rais Magufuli ameyazungumzia katika hotuba yake ni suala la serikali kuhamia Dodoma, ambapo amesema kuwa kabla ya miaka yake mitano ya uongozi atahakikisha yeye na viongozi wote wanaomfuata wanahamia Dodoma ikiwa ni kuonyesha dhamani ya makao makuu ya nchi.

Nolito: Nimeikataa FC Barcelona Kwa Sababu Ya Pep Guardiola
Game Ya Man Utd Vs Man City Yapigwa Kalenda