Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina ametoza faini ya shilingi milioni thelathini  Gereza la keko lililopo jijini Dar es salaam kwa kosa la kutiririsha maji taka kwenye makazi ya watu.

Hatua hiyo ameifikia mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoishi jirani na gereza hilo na kupelekea kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira kwenye gerezani hapo na kujionea uchafuzi na utiririshaji wa maji taka kwenye makazi hayo.

Aidha, Mpina ameiagiza NEMC kutoa maelekezo kwa  mkuu wa gereza hilo kujenga miundombinu ya maji taka ambayo ni rafiki kwa mazingira sambamba na kulipa faini hiyo kwa muda wa wiki mbili.

“Taasisi za Serikali zinapaswa kuwa mfano kwa kutii sheria za nchi hususani sheria ya mazingira nimesha sema mara nyingi na ninarudia hapa tena taasisi za Serikali haziruhusiwi kuchafua mazingira kwa namna yoyote ile kwa mujibu wa sheria. “ alisema Mpina.

Maalim Seif, Mtatiro kufuta nyayo za Lipumba Kusini
Video: Endeleeni kushirikiana na Serikali - Majaliwa