Waziri wa Fedha na Mipango nchini,Dkt. Philip Mpango amesema kuwa kitendo cha kuhujumu uchumi wa nchi na rasilimali za taifa ni kitu ambacho hakivumiliki hata kidogo kwani kufanya hivyo ni unyama na ni ufisadi mkubwa.
Ameyasema hayo mapema hii leo katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Internatinal Airport (JNIA) jijini Dar es salaa kwenye makabidhiano ya ripoti ya madini yaliyozuiwa uwanjani hapo.
Dkt. Mpango amesema kuwa kitendo hicho hakipaswi kuendelea kutokea, huku akiwapongeza wale waliohusika kwenye kufanikisha kukamatwa kwa madini hayo uwanjani hapo ambayo yalikuwa tayari kwaajili ya kusafirishwa.
“Kwa niaba ya Serikali napenda niwashukuru sana sana vyombo vyote ambavyo vimefichua uovu huu, ni unyama, mimi sina lugha nzuri ya kuwaambia mnataka niwaambie nini? ni unyama wa hali ya juu, ni ufisadi, hongereni sana kwa kutusaidia kufichua kujua tunaibiwa sana,” amesema Dkt. Mpango
-
Maaskofu waamua kurudisha fedha za Escrow
-
Bidhaa za nje zasababisha mfumuko wa bei Visiwani Zanzibar
-
Ni bora tuifunge kuliko kuendelea kuibiwa- JPM
-
LIVE BREAKING: Serikali ikipokea taarifa madini yaliyozuiwa uwanja wa ndege DSM
Aidha, ameongeza kuwa zilisalia dakika 5 tu, ili ndege yenye madini hayo iondoke nchini, na ndipo walipoyakamata hivyo kuweza kuokoa kiasi kikubwa cha madini ambayo yangeiingizia hasara Serikali.
Hata hivyo, Madini yaliyokamatwa uwanjani hapo ni aina ya Almasi yenye thamani ya dola za Marekani milioni 29.5 iliyotambulika baada ya serikali kufanya tathmini yake, wakati yalipokamatwa wahusika walisema yana thamani ya dola za Marekani milioni 14. 7