Mwandishi wa Habari na Mmiliki wa ‘DarMpya Blog’, John Marwa amesema kuwa ameshtushwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba kumtaja katika orodha ya watu kumi ambao ni hatari kwa usalama wa taifa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa hajawahi kuwa karibu na watu hao.

Aidha, Marwa amesema kuwa kwasasa anajadiliana na wanasheria wake kuona namna ya kumfikisha mahakamani mkurugenzi huyo ili aweze kuthibitisha tuhuma hizo.

“Kwanza kabisa suala hili limenisikitisha sana, limenijengea taswira mbaya kwa ndugu, jamaa na marafiki hata kwa wafanyakazi wenzangu kwa sababu kila mmoja ananishangaa kutajwa katika orodha hiyo,”amesema Marwa

Hata hivyo, Marwa ameongeza kuwa mpaka sasa bado hajajua kisa cha mkurugenzi huyo kumtaja kwani hajawahi kufanya kosa lolote la kihalifu.

Raia wa kigeni akwepa jela alipishwa mamilioni
Taifa Stars kuzikabili Algeria, DR Congo