Raia wa China, Liu Xiu Feng, amelipa faini ya shilingi milioni 110, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuhukumu kwenda Jela miaka 20 kwa kushindwa kutumikia kifungo hiko.
Raia huyo amelipishwa faini hiyo baada ya kukutwa na meno mawili ya Simba katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mnamo February 7, 2018.
Mahakama imesema kuwa meno hayo yanathamani ya shilingi Milioni 11,029,900.
Hata hivyo Hakimu aliyesimamia kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi amesema kwa maelezo ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi mshtakiwa huyo alikiri kufanya kosa hilo la wizi wa meno hayo ya Simba.
Na ndio sababu iliyompelekea mtuhumiwa kukwepa kifungo cha miaka 20 jela na kukubali kulipa faini hiyo iliyotolewa na Mahakama.

 

Polepole adai ukabila unaikosesha ushindi CCM Mbeya Mjini
Video: John Marwa kumshughulikia Musiba