Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesisitiza kwa mara nyingine kuwa jengo la TANESCO Ubungo ni lazima libomolewe ili kupisha upanuzi wa barabara.
Ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila jijini Dar es salaam.
“Wakati nikiwa Waziri, Mheshimiwa Pinda alinipinga kuhusu kubomoa jengo la TANESCO lakini kwa sasa hawezi kwasababu Mimi ndiye Rais, nilikaa kimya kwasababu ya kuogopa kufukuzwa,”amesema Rais Dkt. Magufuli
Aidha, ameongeza kuwa Jengo hilo lazima libomolewe hata kama nusu yake ndio ipo kwenye hifadhi ya barabara itolewe.
-
Video: Watumishi Tanesco wawekwa kikaangoni
-
Video: Majaliwa amlilia Leonidas Gama, ”ametuachia pengo kubwa…
-
Karia atuma salamu za rambirambi msiba wa Gama
Hata hivyo, amesema kuwa wakazi wa Kimara ambao nyumba zao zimebomolewa hawatalipwa fidia kwasababu zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara.