Chama cha urembo na vipodozi Tanzania (TCA), kinacho tarajia kuzinduliwa rasmi Agosti 26 mwaka huu kimejipanga katika kuleta mapinduzi ya urembo na vipodozi hapa nchini kwa kushirikiana na wadau wote wa sekta ya urembo na vipodozi kama watengenezaji wa bidhaa asilia, waelimishaji na matabibu wa ngozi.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa chama hicho Shekha Nasser ametoa wito kwa wananchi kuhudhuria uzinduzi wa chama hicho utakao fanyika kwenye jengo la PSSSF kijitonyama Dar es salaam ili waongeze ujuzi juu ya urembo na vipodozi kwa wanaume na wanawake.

Kwa upande wa baadhi ya washirika wa chama hicho, Kopa fasta, Datavision iternational, na Sigma hair ind. ltd wameeleza jinsi wanachama wa TCI watakavyo nufaika nao watakapo jiunga…, Bofya hapa kutazama na kujua kwa kina taarifa hii

DPP amfutia mashtaka mkurugenzi wa shirika la Petroli TPDC
Tafuteni suluhu badala ya kushindana- RC Gambo