Kampuni ya DataVision International imejipanga kufanya mambo makubwa zaidi mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maadhimisha ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Teddy Quitu alipokuwa akizungumza na Da24 Media, ambapo amesema kuwa Kampuni hiyo imejikita katika masuala ya Tehama, Takwimu, Utafiti na Kadi za Malipo.

Amesema kuwa Kampuni hiyo ya kizawa imekuwepo tangu mwaka 1998 ambapo inafanya kazi zake hapa nchini na nchi za nje.

“Kampuni hii ya DataVision International imesaidia pakubwa sana kutoa ajira, kuna idadi kubwa sana ya watu wengi sana tulionao na wengine tumewakuza,”amesema Teddy Quitu

Mahakama ya Tanzania yalaumiwa kutotenda haki kesi ya Babu Seya na mwanae
Semakafu atoa mwongozo umri wa mwanafunzi kujiunga kidato cha tano/sita, 2018