Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema jitihada zilizofanywa na kamati ya uokoaji zimefanikiwa kuopoa maiti 224 baada ya kuongezeka mwili mmoja leo na waliohai ni 41 ambao wapo hospitali kwa matibabu zaidi.

Amesema kati ya hao maiti za watu wazima wanawake zimepatikana 126, na wanaume 71, huku watoto wa kike 17, na wakiume 10 jumla inafanya maiti 224.

Na maiti zilizotambuliwa ni 219 na zikiwa zote zimechukuliwa na ndugu, huku maiti 4 tu hazijatambuliwa.

Miili 5 iliyotambuliwa imeungana na Serikali kuzikwa pamoja na ile isiyotambuliwa, hivyo leo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezika marehemu 9.

Aidha, Rais Magufuli aliagiza ndugu wa marehemu wote kupewa pesa taslimu shilingi laki 5 ili ziweze kuwasaidia katika shughuli nzima ya kuwapumzisha marehemu wote.

Video: Serikali kuunda kamati ya uchunguzi ajali ya Mv Nyerere
LIVE: Miili ya Watanzania ikihifadhiwa katika nyumba zao za milele