Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa amesema kuwa wamekamata majambazi waliokuwa na silaha mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumika kufanyia uhalifu.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa msako wa wahalifu unaendelea kufanyia na hauna kikomo.

Aidha, amewataka wananchi wa jiji la Dar es salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ambao wamekuwa wakitoa siku zote ili waweze kutokomeza uhalifu katika jamii.

“Bado msako wa wahalifu unaendelea mpaka tuhakikishe vitendo vya kiovu vinakwisha katika jiji hili, sasa nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano wa taarifa,”amesema Kamanda Mambosasa

Majaliwa awawashia moto watumishi Mara, ataka waishi kwenye vituo vyao vya kazi
Zitto agonga mwamba Kigoma Mjini