Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze amesema kuwa Idara ya Uhamiaji inashikilia hati yake ya kusafiria tangu Julai 24, ambapo licha ya kuwa na hati ya dharura, juzi Agosti Mosi mwaka huu alizuiliwa kusafiri kwenda jijini Nairobi.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa aliitwa uhamiaji na kutakiwa kupeleka hati yake ya kusafiria bila kuwa na taarifa yoyote ya amri ya kimahakama yenye kuidhinisha jambo hilo.
“Niliitwa Uhamiaji nikahojiwa kidogo na kuambiwa nipeleke pasipoti yangu sikuona haja ya kukataa sababu ni haki yao kuchukua, ila hadi sasa sijapata tamko rasmi kwa nini wamechukua,”amesema Eyakuze.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amesema Twaweza wataendele kufanya kazi zao kama kawaida pamoja na changamoto wanazopitia, ikiwamo kutumiwa barua mbili na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ikiwahoji kuhusu uhalali wa programu yao Sauti za Wananchi na kuwataka wafafanue kwanini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao