Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania, Augustino Mrema ameungana na wakristo wote kusherekea sikukuu ya Pasaka.

Aidha, akiwa katika Kanisa Katoliki Sinza, amewaasa waumini kutenda matendo mema ili kuendana na uhalisia.

“Tumekuwa katika kipindi hiki cha mfungo, na leo hii tunafungua kwa kusherekea mateso ya bwana wetu Yesu Kristo aliyoyapata msalabani, hivyo basi nawaasa waumini wenzangu tuishi katika bwana, kwani yeye ndiye uzima wetu,”amesema Mrema.

Aidha, Katika hatua nyingine Mrema amechangia kiasi cha shilingi Milioni moja kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Kanisa hilo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ni vyema kila mtu kumcha Mungu ili kuweza kulinusuru taifa na matendo maovu ambayo yanazidi kujitokeza.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 17, 2017
JPM atoa zawadi ya Pasaka kwa makundi yasiyojiweza