Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka kuchukua hatua kali kwa wote waliohusika na upotevu zaidi ya sh. bilioni moja za vyama vya ushirika.

Majaliwa amesema hayo Januari 27, 2017 alipozungumza na watumishi wa Mkoa wa Njombe wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku saba mkoani hapa.

Amesema kati ya fedha hizo sh. milioni 532.736 zilipotea katika SACCOS ya Kurugenzi  Njombe pamoja na sh. milioni 900 zilizopotea katika Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kiitwacho Wafanyabiashara Njombe SACCOS.

“Maofisa Ushirika nchini mmeendelea kudhoofisha jitihada za Serikali katika kuimarisha ushirika. Katika eneo hili ninahitaji Mkuu wa Mkoa ufuatilie suala hili na kuwachukulia hatua wahusiuka wote,” alisema.

Majaliwa amewaagiza Wakuu wote wa Wilaya kuwatumia warajisi wa ushirika kuimarisha ushirika Mkoani Njombe, amesema ”Tunataka ushirika ulete tija kwa wananchi na hatutaki ushirika ulioambatana na harakati za kugawa watu. Endeleeni kuwashughulikia wanaushirika wasio waaminifu,”.

 

 

Agizo la JPM lazua tafrani chadema,makada wawili nusu wachapane makonde
Daktari feki chanjo ya kimataifa adakwa akitoa huduma hospitali ya Mnazi mmoja