Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa mbali na vita ya dawa za kulevya inayoendelea, sasa hivi limeibuka jambo kubwa zaidi ambalo lisiposhughulikiwa litakuwa na madhara makubwa sana katika jamii.

Kamishna Sirro amesema kuwa kuna mazoezi ya Judo, Kareti, kujifunza silaha kwenye nyumba za ibada na kupelekea watoto wadogo kuacha kusoma badala yake wanajifunza matumizi ya silaha misituni hali ambayo itakuwa na madhara makubwa kwenye jamii.

Amesema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya mauaji yanayotokea sehemu mbali mbali ambapo jeshi la Polisi linaendelea kupambana na changamoto hizo na kutoa taarifa za matukio hayo, hivyo amewataka viongozi wa dini kutoa taarifa na kutunza waumini wao na kuwaepusha na mafunzo hayo hatarishi.

Ni Zamu Ya Ligi ya Europa kutimua tena
Rashford kulamba dume au garasa Kikosi cha England?