Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeondoa utaratibu wa awali kwa walipakodi wadogo kulipia kodi kabla ya kuanza kufanya biashara na badala yake kuwataka kulipia robo ya kwanza ndani ya siku tisini tangu kusajiliwa.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya alipokuwa akizungumza na waadishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu uzinduzi wa kampeni ya usajili wa walipakodi.
Amesema kuwa jukumu la usajili wa walipakodi kwa Mamlaka hiyo ni chanzo cha kuongeza idadi ya walipakodi, wigo wa ulipaji kodi, kuongeza makusanyo pamoja na kuwa na taarifa sahihi za walipakodi wanaostahili kukadiriwa na kutozwa kodi ili kuchangia Pato la Taifa.
“kampeni hii inaenda sambamba na mabadiliko makubwa tuliyoyafanya kwa walipakodi wadogo kwa kuwapa siku tisini za kulipa kodi kwa robo ya kwanza ya malipo pindi tu watakapokuwa wamesajiliwa hivyo mabadiliko hayo yatakuwa chachu katika usajili kwani tunatarajia kusajili walipakodi takribani milioni moja nchi nzima,”amesema Mwandumbya.
-
TRA: Hatuhitaji kulumbana na Askofu Kakobe
-
Kisa cha raia wa kijerumani kuuawa kwa kisu Zanzibar
-
TCRA yawalima faini Star TV, Azam TV kuhusu uchaguzi wa madiwani