Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Natalie Boucly wamekubaliana kuanzisha kikosi kazi cha pamoja cha kuchunguza tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON kuhusu ujangili wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa.
 
Dkt. Kigwangalla na Mkurugenzi huyo, wamefikia makubaliano hayo leo wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii zilizopo Jijini Dar es Salaam.
 
Aidha, Waziri Kigwangalla amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Wizara yake inaandaa mikakati mbalimbali ya kuongeza idadi ya watalii nchini na mapato ikiwemo kuwashirikisha wananchi kuandaa mwezi maalum wa Urithi wa Tanzania pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa njia za kielektroniki katika vituo mbalimbali ya Utalii.
 
  • TCRA yawalima faini Star TV, Azam TV kuhusu uchaguzi wa madiwani
  • Kisa cha raia wa kijerumani kuuawa kwa kisu Zanzibar
  • TRA: Hatuhitaji kulumbana na Askofu Kakobe
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo amemuahidi Waziri Kigwangalla kuendelea kumpa ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kuendeleza Utalii nchini na uhifadhi wa misitu na wanyamapori kwa ujumla
Benki ya dunia yazidi kuineemesha Tanzania
Video: TRA yabadili utaratibu wa ulipaji kodi