Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema amefurahishwa sana na kikosi chake kwa ushindi walioupata wa magoli 2 – 0 dhidi ya Chelsea. Amesema furaha yake hiyo isiyo na kifani si kwa sababu ni kikosi chake kimeifunga Chelsea, ni kwa sababu walihitaji alama hizo tatu.

“Sihisi furaha zaidi kwa sababu ya kuifunga Chelsea, tuliwafunga viongozi wa ligi. Haijalishi kama kiongozi wa ligi ni Chelsea au klabu nyingine, tuliwachapa vizuri.”

Mourinho amesema kuwa hakuna anayeweza kusema Manchester United haikustahili kushinda mechi hiyo, hivyo amefurahishwa na kikosi chake kwa kufanikiwa kuwadhibiti viongozi wa ligi ya England Chelsea na kuwalaza 2-0 katika uwanja wa Old Trafford.

Manchester United ilifungwa na Chelsea 4-0 mechi ya kwanza msimu huu ugenini, Stamford Bridge na pia ilishindwa robo fainali katika Kombe la FA pia uwanjani Stamford Bridge.

Mourinho hakukubali tena kuzidiwa wakati huu ambapo aliwapanga pamoja Marcus Rashford na Jesse Lingard safu ya mshambulizi na akampumzisha Zlatan Ibrahimovic.

Rashford alitangulia kufunga na Ander Herrera, ambaye alimdhibiti vilivyo Eden Hazard ,alifunga la pili kipindi cha pili.

Kufuatia ushindi huo, Mourinho amesema kuwa anampango ule ule wa wachezaji 11 ambao ulifanya kazi katika Kombe la FA uwanjani Stamford Bridge. Ndio bora zaidi kwa kucheza kaunta kote nchini na tuliwadhibiti vilivyo.

 

United watakuwa wenyeji wa Anderlecht mechi ya marudiano Europa League Alhamisi, na watarejea katika ligi kucheza dhidi ya Burnley Jumapili, ambapo Chelsea nao watakutana na Tottenham nusu fainali Kombe la FA Jumamosi ijayo.

Twiga maarufu Duniani azaa
Video: Marekani yasema haitakuwa na subira tena dhidi ya Korea Kaskazini