Wabunge nchini Uganda wamepigana ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa katika siku ya pili ya kikao cha kujadili muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea nafasi ya urais kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo.

Ugomvi huo ulianza pale Spika alipochukua hatua ya kuwafukuza wabunge 25 wengi wao wakiwa ni wale wa upinzani kwa madai ya utovu wa nidhamu pamoja na waziri wa serikali aliyeshtakiwa kwa kufyatua risasi bungeni siku ya jumanne.

Wabunge nchini humo wanadai kuwa kama kikomo cha umri wa miaka 75 kitaondolewa basi rais aliyepo kwa sasa atapata nafasi ya kugombea tena mwaka 2021 kitu ambacho wapinzani hawataki.

Katika ugomvi huo wabunge hao walirushiana viti, kuharibu vipaza sauti katika kikao hicho kilichoongozwa na Spika wa bunge Rebecca Kadaga.

Tazama kilichotokea katika video hii hapa chini;

Video: JPM aiteka UN, Askofu ajitoa mhanga kilio cha Katiba Mpya
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 28, 2017