Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewataka madalali wote nchini kuacha mara moja tabia ya kuwanyonya na kuwatapeli wanyonge kupitia mikopo mbali mbali wanayokopa kutoka kwenye mabenki mbalimbali hapa nchini na kusema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakaye bainika kufanya hivyo.

Waziri Lukuvi amesema hayo leo Oktoba 5, 2016 wakati akizungumza na madalali hao ofisini kwake jijini Dar es salaam ambapo ametoa maelekezo kwa kile kinachotakiwa kifanyike  ili kuondoa matatizo yanayojitokeza.

Lukuvi amesema kuwa kuna kesi zaidi 87 zilizopo mezani kwake ambazo zimesababishwa na madalali, kesi za viwanja, watu kuuziwa nyumba zao kwa gharama ambazo haziendani na thamani husika. Bofya hapa kutazama video

Tyson Fury Akiri Kutumia Cocaine
Hafla Ya Kuwapongeza Serengeti Boys