Manispaa ya Ilala imetenga masoko matano (5) kwaajili ya Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa jina la machinga ambao wamekuwa wakifanya biashara zao katika mazingira magumu, masoko hayo ni pamoja na Kigogo Fresh, Kivule kerezange, Kivule center, Kinyerezi na Tabata, huku Kigogo Fresh na Kivule kerezange yakiwa yamekamilika tayari kwaajili ya kutumika.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema alipokuwa akizungumza na wafanya biashara ndogo ndogo maarufu kwa jina la machinga eneo la Gerezani Kariakoo jijini Dar es salaam na kutembelea masoko hayo, pia Mjema ametoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mpango huo wa kuwapeleka machinga katika masoko hayo.

Mjema amesema mpango huo utawanufaisha wafanyabiashara hao na Serikali kwa ujumla kwa kukusanya mapato yatokanayo ushuru wa kodi, pia utawafanya wawe rasmi katika maeneo hayo na kuondokana na adha ambayo wamekuwa wakiipata.

Aidha ameongeza kuwa Manispaa zingine za jiji zimetenga maeneo kama hayo kwaajili ya wafanya biashara hao na kuwataka wale wote wanaotoka katika manispaa hizo kufanya biashara zao katika manispaa zao ili kupunguza msongamano katikati ya jiji.

Live: Maswali na majibu kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma
Patrick Vieira: Wenger Hakunisisitiza Kuwa Meneja