Rais wa Kenya, William Ruto amekiri kuwa Serikali inatakiwa kulaumiwa katika maujai yaliyotokea eneo la Shakahola huko Malindi kaunti ya Kilifi, ambayo yaliwahusisha waumini wa Kanisa la Good News International Church, la Mchungaji Paul Mackenzie.
Rais Ruto aameyasema hayo wakati akiongea na vyombo vya Habari nchini humo na kuongeza kuwa anaomba msamaha kwa wakenya, kutokana na vitengo vyote vya serikali hasa idara ya usalama kuwa usingizini.
Mchungaji wa Kanisa la Good News International Church, Paul Mackenzie. Picha ya Citizen Digital.
Amesema, “vyombo vya ulinzi, vitengo vyote vya Serikali hasa idara ya usalama vilikuwa na utepetevu, katika kutambua mapema na kuzuia mauaji hayo, hivyo wa kulaumiwa katika hili ni Serikali na niwaombe msamaha wakenya.”
Mapema hapo jana (Mei 15, 2023), Mamlaka za Serikali nchini humo zilisema idadi ya waliofariki katika mkasa huo imeongezeka hadi kufikia watu 201, huku timu ya uokoaji ikisema imepata miili 22 zaidi katika msitu wa pwani.