Mawaziri wa Uwekezaji wa Tanzania na Kenya, wametakiwa kukutana na kwa mazungumzo na kuhakikisha wanaondoa vikwazo 14 vya kibiashara, vilivyobaki kati ya vikwazo 64 vilivyoainishwa kuleta mkanganyiko baina ya nchi hizi mbili za Afrika ya Mashariki.

Wakiongea kwa nyakati tofauti hii leo Oktoba 10, 2022 katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa upande wa Rais Samia amesema uamuzi huo ni miongoni mwa mambo waliyojadiliana ili kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Kazi hii ilianza na Rais Mstaafu, Uhuru Kenyata na tulikubaliana kwa kuwataka wataalamu wetu kufanyia kazi vikwazo vya biashara vilivyopo ambapo Mawaziri wetu walitambua vikwazo 68 na vilifanyiwa kazi 54 sasa tumewataka wakutane na kufanyia kazi vikwazo hivyo ili kuwe na uhuru wa kibiashara.”

Rais Samia akizungumza na Rais Ruto.

Kwa upande wake Rais wa Kenya, Willam Ruto amesema biashara baina ya nchi hizi mbili imezidi kuimarika, ambapo usafirishaji wa bidhaa kwa mwaka mmoja imepanda kutoka Sh. 27 bilioni kutoka Tanzania na kufikia Sh. 50 bilioni kwenda Kenya na usafirishaji wa bidhaa kutoka Kenya kuja Tanzania ukipanda kutoka Sh. 31 bilioni kufikia Sh. 45 bilioni.

Amesema, “Leo tunanunua vitu vingi kutoka Tanzania kuliko wanavyonunua kutoka Kenya na hii ni kutokana na ushirikiano baina ya nchi zetu na biashara kati ya nchi hizi mbili zinainufaisha Tanzania zaidi kuliko Kenya.”

Hata hivyo, Rais Ruto amesema Mawaziri baina ya Kenya na Tanzania wanapaswa kufanyia kazi changamoto zilizobaki na kuwahimiza hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu changamoto zote ziwe zimetatuliwa.

Killy na Cheed 'watupiwa virago' Konde Gang
Misri na Ugiriki 'zawashtukia' Uturuki na Libya