Zoezi la makabidhiano ya Ofisi na nyaraka muhimu kati ya Kamati ya Mpito iliyokuwa ikiongoza Soka la Zanzibar na Kamati Tendaji ya Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFA) iliyokuwa ifanyike leo, imeingia baada ya vurugu kuzuka katika ofisi za Shirikisho hilo.

Vurugu hizo zilipelekea Jeshi la Polisi kuingilia kati na kuuondoa ulinzi wa raia wenye misuli na miraba minne maarufu kama ‘mabaunsa’ katika ofisi za Taifa Aman, Unguja.

Taarifa kutoka visiwani humo zimeeleza kuwa, wakati wajumbe wanakwenda katika ofisi ya chama hicho ndipo walipokuta ofisi hiyo imezungukwa na watu wasiojulikana ambao ni ‘mabaunsa’, jambo ambalo limepelekea Kamati tendaji ya ZFA Taifa kuwaita Jeshi la Polisi na kuwashughulikia watu hao.

Baada ya Jeshi la Polisi kufika Amani kwenye ofisi za chama hicho majira ya saa 6 mchana, lilifanikiwa kuwakamata baadhi ya watu waliokuwa wanalinda ofisi hiyo.

Ndani ya Ofisi hiyo alikuwemo Massoud Attai ambayee ni mjumbe kamati tendaji akiwakilisha Wilaya ya Kaskazini “A”,, ambaye alitolewa baadae na kuruhusiwa kuondoka.

Mussa Suleiman Soraga ambaye ni mjumbe wa ZFA Taifa akitokea Wilaya ya Magharibi “A” ameelezea tukio hilo wakati akiongea na wana habari.

“ Kwa masikitiko makubwa tunasikitika, tumekuta walinzi zaidi ya 40, yani mabaunsa wanalinda hapa ZFA, sisi tukaripoti polisi kama ZFA imevamiwa na watu wasiojulikanwa, wakaja polisi wakawakamata na wengine wakakimbia, ofisi ndani alikuwemo Attai akambiwa atoke na Jeshi la Polisi akatuachia ofisi yetu lakini ufunguo katuambia anazo Hussein , ila sisi tumeshanunua kufuli jipy,”alisema.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito, Hussein Ali Ahmada ambaye kamati yake ilitakiwa leo kwenda kukabidhi ofisi na nyaraka za chama hicho amesema hakuwa na taarifa za kuwepo kwa makabidhiano ya ofisi leo hii, huku akikana kuwa na funguo za ofisi za ZFA.

 

Chanzo cha Maalim Seif kukimbizwa hospitali ghafla chawekwa wazi
Sakata la kusimamishwa Wauguzi Butimba, madaktari wagoma