Mabingwa wa soka Tanzania bara, Young Africans wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo, Yanga italazimika kwenda kushinda ugenini ili kutimiza ndoto za kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya pili katika historia yao baada ya mwaka 1998.
yanga01

Katika mchezo wa leo, mabao yote yalipataka kipindi cha kwanza, Ahly wakitangulia kufunga kupitia kwa mshambuliaji wake mjanja, Amr Gamal, kabla ya Yanga kusawazisha la ‘ngekewa’ la Issoufou Boubacar.

Picha: Manny Pacquiao Amshinda Brandley, Ampiga Chini mara mbili
Azam FC Kuwakosa Kapombe, Sure Boy