Waziri wa kilimo, Japhet Hasunga ameagiza wakala wa hifadhi ya chakula nchini (NFRA) kufanya utafiti wa kina katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ili wananchi waweze kupelekewa chakula kwa gharama nafuu.

Ametoa maagizo hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua bodi ya ushauri ya NFRA. 

Aidha ameitaka NFRA kubainisha malengo na vipaumbele vyake vya akiba ya hifadhi ya chakula katika kipindi hiki ambacho taifa linakabiliwa na janga la maambukizi ya virusi vya corona.

Mpaka hivi sasa Nchini Tanzania kuna wagonjwa takribani mia tatu waliopata maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkwasa awahimiza wachezaji Young Africans
Rage hachoki kuwatania Young Africans