Wabunge wameitaka Serikali kutoa maelezo ya Dola milioni 300 za Marekani  (sawa na Sh570 bilioni) zilizotolewa na wahisani kusaidia miradi ya afya, lakini hazijatumika.
Fedha hizo zilitolewa na Global Fund kugharimia miradi ya ukimwi, malaria na kifua kikuu (TB) na zinatakiwa hadi Desemba mwaka huu ziwe zimeshatumika.
Mjadala huo ulizuka katika semina ya wabunge wa kamati tatu za Bunge kuhusu afya ya wanawake, watoto na vijana iliyoandaliwa na Umoja wa Mabunge ya Dunia (IPU) na Bunge la Tanzania.
Semina hiyo imeshirikisha Kamati ya Bajeti,  Huduma na Maendeleo ya Jamii na ya Masuala ya Ukimwi.
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Suzan Lyimo amesema bila kuwa na bajeti ya kutosha, malengo ya pambano dhidi ya ukimwi hayawezi kufikiwa.
“Tunasikia kuna wadau wengi waliokuwa wanasaidia eneo hili wamejiondoa. Nataka kufahamu wanasemaje kuhusu hili?” amesema Lyimo.
Akijibu hoja hiyo, Mariana Balampama kutoka Kundi la Washirika wa Maendeleo (DPG), amesema wafadhili hawajajitoa kusaidia miradi hiyo.
Balampama amesema Marekani na Global Fund wanaendelea kutoa misaada na kwamba, muda wa matumizi ya fedha zilizotolewa na Global Fund unakaribia kuiisha na hazijatumika

Polisi waingilia kati sakata la Askofu Mokiwa
Mpoto aunga mkono mapambano madawa ya kulevya, ampongeza Makonda