Matokeo ya Ubunge yanaendelea kutangazwa na wasimamizi katika majimbo mbalimbali ambapo jimbo la Iringa Mjini, Temeke, Kibamba na Kawe wamepata majibu ya wawakilishi wao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Matokeo rasmi yaliyotangazwa na wasimamizi yanaonesha kuwa Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema ameweza kutetea kiti chake na kuwa tena mbunge wa jimbo la Iringa Mjini.

Jimbo la Temeke limeshuhudia mabadiliko ambapo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Abbas Mtemvu wa CCM amepoteza nafasi hiyo baada ya msimamizi kumtangaza Abdallah wa CUF kuwa mbunge mteule wa jimbo baada ya kupata kura nyingi zaidi.

Sauti ya wapiga kura wengi zaidi wa jimbo jipya la Kibamba imesikika na msimamizi amemtangaza John Mnyika kuwa mbunge wa jimbo hilo jipya.

Katika Jimbo la Hanang, Dkt Mary Nagu ametetea kiti chake na anaendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Katika hatua nyingine, CCM imeweza kuthibisha kuwa Dodoma bado ni ngome yake kubwa baada ya kushinda ubunge katika majimbo yote 10.

Stephen Masele ametangazwa kuwa mshindi katika jimbo la Shinyanga Mjini.

Ukawa Wapinga Mwendendo wa Matokeo ya Urais, wataka vijana wao Waachiwe
Wassira: Sikubali, Nimehujumiwa