Mwanamke mmoja nchini Kenya anusurika kubakwa na wanaume watatu baada ya kuwadanganya wanaume hao kuwa ni muathirika wa ukimwi.

Wanaume hao walimdhalilisha mwanamke huyo wakiwa ndani ya basi la abiria kwa kumvamia, kumvua nguo na kumwibia baadhi ya mali alizokuwa nazo.

Hivyo mahakama imeamuru hukumu ya kifo kwa wanaume hao kwa tuhuma za wizi wa kutumia nguvu.

Tukio hilo limetokea miaka mitatu iliyopita ambapo watu walilirekodi  na kulisambazwa katika mitandao ya kijamii.

Wanaume hao watatu ni dereva wa basi Nicholas Mwangi, na makondakta wake Meshack Mwangi na Edward Ndung’u.

Hakimu wa Nairobi Francis Andayi, amesema kuwa kitendo hicho kilikuwa kibaya lakini watuhumiwa hao walioonekana kufurahia walichokuwa wanafanya kwa sababu walikuwa wakishangilia huku wakimvua nguo mwanamke huyo.

Kupitia video hiyo iliyosambaa mitandaoni ya mwanamke aliyetaka kubakwa na wanaume watatu mamia ya wanawake nchini Kenya wamefanya maandamano kupinga vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.

 

Magazeti ya Tanzania leo Julai 20, 2017
Mambosasa: Hatuna mpango wa kumkamata Lissu