Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameongeza zuio la watu kukaa ndani kwa majira ya usiku kwa mwezi mmoja, ambapo kwa sasa muda wa zuio hilo utaanza saa 3 usiku mpaka saa 10 alfajiri badala ya saa 1 usiku hadi saa 11 alfajiri.

Ametoa tangazo hilo wakati akibainisha kuwa idadi ya maambukizi nchini humo imeongezeka kufikia 2,600 baada ya Wagonjwa wapya 126 kuongezeka.

Aidha, ametangaza kuwa masomo yatarejea kuanzia Septemba 1, 2020 ambapo Wizara ya Afya na ile ya Elimu zitafanya mazungumzo ili kutoa mwelekeo wa jinsi Wanafunzi watarudi shuleni.

Pamoja na hayo, mikusanyiko ya hadhara ikiwemo ya kisiasa bado inaendelea kuzuiliwa pamoja na baa hadi pale Serikali itakapotoa maelekezo zaidi

Mtandao kusaidia maonesho ya sabasaba 2020
Grealish na Havertz wavutana Manchester United