Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi nchini, Sudi Mwakibasi amesema wakimbizi wameanza kuingia nchini tangu machi 5 mwaka huu (2023), na kwamba idara hiyo inapokea kwa wastani kati ya watu 100 hadi 300 wanaongia nchini, wakitokea nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC.

Mwakibasi amesema kuwa, kinachofanyika kwa sasa, ni Tanzania kutekeleza hitajio la msingi la kuwapokea wanaohitaji hifadhi na kueleza kuwa, kundi hilo linahusisha wakimbizi wapya walioingia moja kwa moja kutoka DRC pamoja na waliokuwa wakiishi nchini bila vibali.

Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi nchini Tanzania Sudi Mwakibasi.

Mkoa wa Kigoma, hadi sasa unahifadhi wakimbizi wapatao laki mbili kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Burundi.

Mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini, yamesababisha idadi kubwa ya watu kuyakimbia makazi yao na kuzidisha mivutano ya kikanda, huku serikali ya DRC ikiishutumu Rwanda kwamba, inawaunga mkono waasi wa M23, madai ambayo yanakanushwa vikali na serikali ya Kigali, ingawa yanaungwa mkono na madola ya Magharibi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi – UNHCR, limesema limesikitishwa sana na kuendelea mapigano makali kati ya makundi ya wanamgambo yenye silaha na vikosi vya serikali yanayowafanya mamia kwa maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao Mashariki mwa nchi.

Nimechoka kusubiri, nitagombea urais: Mtoto wa Rais Museveni
Zanzibar kupima ubora wa Bidhaa kwa viwango vya Kimataifa