Wakimbizi 46 wamefariki dunia ndani ya Lori ambalo limetelekezwa nje kidogo ya jiji la Texas nchini Marekani, huku zaidi ya wengine 16 wakiwemo watoto 4 wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Meya wa Mji wa San Antonio, Texas Ron Nirenberg amenukuliwa akisema ”Polisi wa zimamoto walifika eneo la tukio na kutoa msaada kwa manusura huku miili yao ikiwa ya moto kutokana na kuathiriwa kwa joto kali.

“Walikuwa na watoto nadhani walikuja kwa ajili ya kutafuta maisha mazuri, ni janga kubwa sana na la kutisha kwa binadamu,”

Mkuu wa kitengo cha zimamoto katika Mji huo Charles Hood amesema “Hatutakiwi kufungua Lori na kuangalia miili iliyogandamana humo, wote sisi tumekuja kufanya kazi pasipo kutegemea kuona hiki tulichokiona,”

Aidha amesema kuwa Lori hilo lililokuwa limetelekezwa halikuwa na huduma ya hewa wala huduma ya maji.

Watu wanaofanya biashara za kusafirisha binadamu mara nyingi hutumia Malori kwa ajili ya kuwasafirisha wakimbizi wasio na vibali mara tu wanapofanikiwa kuingia ndani ya nchi ya Marekani.

Simba SC, Young Africans zategwa Ngao ya Jamii 2022
Cesar Manzoki amaliza ubishi Instagram