Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad jana alifanya kikao cha faragha na viongozi wa Ukawa kilichohudhuriwa na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na hatua za kuchukua.

Kikao hicho cha siri kilihudhuriwa na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu na Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Twaha Taslima.

Baada ya kikao hicho, Profesa Baregu aliwaambia waandishi wa habari kuwa lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili hatua stahiki za kuchukua kufuatia mkwamo wa mazungumzo ya kutafuta maridhiano.

“Mgogoro wa Zanzibar ni Mkubwa. Kwahiyo tumejadili kuamua tuendelee wapi katika kutatua mgogoro huo,” alisema Profesa Baregu na kuongeza kuwa hakuna makubaliano rasmi ambayo yamefikiwa jana.

Taarifa nyingine zilizopatikana zimeeleza kuwa viongozi hao wamepanga kukutana tena mjini Dodoma kuzungumza na wabunge.

Walimu wapigwa marufuku kupaka lipstick, wanja
Israel yamwagia sifa Rais Magufuli, yaahidi ushirikiano