Wananchi Mkoani Njombe wameshauliwa kufuga Ng’ombe wa maziwa kwa wingi sambamba na kuwapa watoto maziwa ili kuunga mkono juhudi za serikali pamoja na kukabiliana na tatizo la udumavu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri wakati wa ziara yake ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa kupitia mradi wa unywaji maziwa uliofadhiliwa na shirika la Heifa International.

“Tuwape watoto wetu maziwa kwani maziwa ni muhimu kwa afya za watoto wetu na hii itasaidia kukabiliana na tatizo la udumavu ambalo ni tatizo kwa sasa, ili kufanikisha jambo hili tunapaswa pia kufuga Ng’ombe wa maziwa,”amesema Msafiri

Aidha amewataka wananchi kuunga mkono juhudi za serikali kwenye uanzishaji wa viwanda na kuongeza kasi ya ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa kwa wingi pamoja na kuunda vikundi vya ushirika vya wafugaji ili kusaidia kupata soko kamili na ili kuliongezea  pato la taifa.

Hata hivyo, kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Uwemba, Robert Ngimbudzi amesema kuwa kuna changamoto nyingi ambazo wanakumbana nazo juu ya mfumo huo.

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 19, 2018
Mwizi wa fedha kwa njia ya mtandao anusurika kifo