Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amewataka wazanzibari kujipangana kushiriki ipasavyo katika
mchakato wa katiba muda utakapowadia ili kuweza kuyasemamea vyema masuala mbali mbali kwa maslahi ya Zanzibar.
Othman ameyasema hayo huko katika Viwanja vya Garagara wilaya ya Mgharibi ‘A’ Unguja alipozungunza katika Mkutano wa hadhara wa chama hicho ulioelezea juu ya masuala mbali mbali
yanayohusu maendeleo ya Zanzibar.
Amesema, wananchi ni lazima watimize wajibu wao huo katika kuhakikisha wote wanashiriki kikamilifu kwenye mchakato huo wa katiba kwakuwa hakuna mtetezi wa maslahi ya Zanzibar bila
wazanzibari wenyewe.
Aidha, Othman amefahamisha kwamba suala hilo la mchakato wa katibani fursa muhimu kwa wazanzibari katika kuyasemea na kutetea mambo muhimu yanayohusu Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hasa ikizingatiwa kwamba fursa hiyo ilishindikana mwaka 2014.
Hata hivyo, Othman amesisitiza kwamba hatua itasaidia sasa kupatikana kwa Zanzibar mpya yenye mamlaka kamili ambayo ndio utajiri wa nchi katika kufikia malengo mbali mbali ya kimaendeleo kupitia uwezo wa kuamua na kutekeleza masuala ya miradi mbali mbali kwa maslahi ya nchi.
Kuhusu suala la Muuungano na Mamlaka ya nchi, Othman, amesema kwamba hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kupiga hatua bila ya kuwepo mamlaka na kwamba suala hilo la mchakato wa katiba liwauanganishe wazanzibari katika kutetea wanayoyahitaji kuwepo ndani ya Muungano.