Taarifa ya Idara ya huduma za dharula Nchini Afrika Kusini, imesema Watu wanane wakiwemo watoto wanne wamefariki ya kupigwa na shoti ya umeme katika matukio mawili tofauti, baada ya siku kadhaa za mvua kubwa kusababisha mafuriko katika makazi duni karibu na mji wa Cape Town.

Taarifa hiyi imeeleza kuwa, Nyumba nyingi katika vitongoji duni vya nje ya mji wa pili kwa ukubwa nchini Afrika Kusini, vina umeme ambao watu hujiunganishia wenyewe nyumba zao au vibanda kwenye waya za umeme zilizo karibu yao ambazo ni haramu na hatari, lakini zimeenea karibu mahali pote.

Aidha, madhara hayo yalisababishwa na Kimbunga ambacho kilipiga eneo la mji wa Cape Town na sehemu kubwa ya mkoa wa Western Cape kwa siku tatu, iliyosababisha mito kupasua kingo zake na kutokea kwa mafuriko kwenye maeneo ya makazi na barabara kuu kote katika mikoa ya Pwani na Bara.

Hata hivyo, zaidi ya wateja 80,000 katika Mkoa wote hawakuwa na umeme kutokana na hali mbaya ya hewa, ambayo ilisababisha umeme kukatika, lakini baada ya mvua kupungua, idadi hiyo ilipungua na kufikia watu 15,000 ambao hawakuwa na umeme hadi jana Septemba 26, 2023.

Majaribio uendeshaji SGR kuanza Desemba
Ongea nao yazinduliwa na ujumbe muhimu kwa Vijana