Hatma ya wachezaji wanaotaka kuendelea ama kuachana na klabu ya Africans Lyon itakayoshiriki ligi daraja la kwanza msimu ujao ikitokea ligi kuu, itafahamika juma hili baada ya mkutano wa viongozi wa bodi ambao utafanyika jijini Dar es salaam.

Kaimu katibu mkuu wa African Lyon, Ibrahim Mohamed amesema azma hiyo imepangwa kuchukuliwa na uongozi kwa lengo la kutoa uhuru kwa wachezaji ambao hawatokua tayari kuendelea na klabu hiyo yenye maskani yake makuu jijini Dar es salaam.

“Tutakutana juma hili na maamuzi ya kikao cha bodi yatatoa ruhusa kwa kila mchezaji anaetaka kubaki ama kuondoka afanye hivyo,”

“Lengo letu tumedhamiria kuona watu wakicheza soka na sio kuwabania, tutafahamu wachezaji tutakaoendelea nao kwa ajili ya kupambana katika ligi daraja la kwanza kwa msimu ujao, ili tufanikishe mpango wa kurudi ligi kuu.” Amesema Ibrahim Issa.

Hata hivyo Ibrahim ametumia nafasi ya kuzungumza na Times FM kwa kuwataka radhi mashabiki wa African Lyon kwa kitendo cha klabu yao kushuka daraja.

“Tunawaomba radhi mashabiki wetu wote, kilichotokea ni hali ya kawaida katika soka, hatukudhamiria kuwa sehemu ya timu zilizoshuka daraja, lakini tunawasisitiza waendelee kuwa na timu yao na tunawaahidi hatutowaangusha tena.”

Klabu nyingine zilizosbhuka daraja sambamba na African Lyon ni JKT Ruvu na Toto Africans.

Hector Bellerin Ajitega Kwa Kauli Yake
Jay Z, Nas wawaongezea kiu mashabiki