Jumla ya Wanawake wanaokadiriwa kufikia 80 wametekwa nyara katika siku za Alhamisi na Ijumaa ya wiki jana (Januari 12-13, 2023) katika maeneo tofauti ya mji wa Arbinda, uliopo Sahel kaskazini mwa nchi ya Burkina Faso.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, kundi la kwanza la wanawake arobaini walitekwa nyara siku ya Alhamisi na jingine la watu ishirini, siku iliyofuata na kwamba wengine walifaulu kukimbia na kisha kutoa taarifa hiyo.

Shahidi anayefanya kazi katika usalama wa eneo la Arbinda, amefichua kuwa “Kwa kweli, vikundi vitatu vya wanawake vilitekwa nyara huko Boukouma, Wourougoudou na Trignaen, yaani sawa na wanawake 80 waliotekwa nyara.”

Tayari, tarifa hiyo imethibitishwa na mamlaka za Burkina Faso kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ikisema sio vikundi viwili bali ni vitatu vya wanawake ambao walitekwa nyara katika maeneo matatu ya Boukouma, Wourougoudou na Trignien.

GGML yaongeza udhamini Geita Gold FC
Serikali kuja na mpango bora wa matumizi ya ardhi