Baraza la wanawake la Chadema (Bavicha) limewahimiza wanawake kuhakikisha wanakaa umbali wa mita 200 kulinda kura zao baada ya kupiga kura kwakuwa ni haki yao.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Bawacha Taifa, Kunti Yusuph alipokuwa akiongea na akina mama katika mkutano mkubwa uliofanyika jijini Mwanza hivi karibuni, katika ofisi za Kanda ya Ziwa za chama hicho.

Bi. Kunti ambaye ndiye mratibu wa mikutano ya Mke wa mgombea urais wa Chadema, Mama Regina Lowassa aliwaambia wanawake hao kuwa kulinda kura ni haki yao kama ilivyokuwa mwaka 2010 na kwamba kinachofanyika mwaka huu ni mbinu za CCM kusingizia hali ya usalama.

“Katika Taifa lolote lile haijawahi kutokea kwamba ukipiga kura uende nyumbani, ndiyo mara ya kwanza kuona kwa Tanzania, hatuwezi kuondoka tutabaki mita 200,” alisema Kunti.

Naye Regina Lowassa aliwataka wanawake hao pamoja na wanawake wengine nchi nzima kutoogopa kufanya mabadiliko na kupuuzia matusi yanayotolewa na CCM katika majukwaa ya kampeni.

“Kama CCM wana nia njema na watanzania, kwa nini wasimame jukwaani na kuanza kutukana ninawaomba Wanawake msitishike na watu wa aina hiyo.”

 

Laana Ya Ufisadi Yaendelea Kuitafuna FIFA
Lazar Markovic Afungaka Kuhusu Brendan Rodgers